Friday, December 21, 2012

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2012 YATANGAZWA

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa leo ametangaza matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2012 uliofanyika nchini kote  tarehe 19 na 20 Septemba, 2012.   

Katika Mtihani huo Jumla ya wanafunzi 894,881 walisajiliwa kufanya mtihani huo ambapo   wavulana ni  426,285 sawa na asilimia 47.64  na wasichana ni 468,596  sawa na asilimia 52.36. Aidha, kati ya  wanafunzi hao, wapo wanafunzi 874,379  ambao walitarajiwa kufanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili na wanafunzi 20,502 walitarajiwa kufanya kwa lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo waliyoitumia kujifunzia.  

Wanafunzi wasioona waliosajiliwa kufanya mtihani ni 92 wakiwemo wavulana 53 na wasichana 39.  Watahiniwa wenye uono hafifu ambao huhitaji maandishi makubwa ni 495, kati yao wavulana ni 238 na wasichana ni 257.


No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...